Kozi

MBC inafundisha kozi nne.

  • Diploma of Theology: 3 Year course in English.
  • Kozi ya Hati katika Theologia: Kwa kiswahili na miaka mitatu.
  • Kozi ya Uinjilisti: Kwa kiswahili na mwaka moja tu.
  • Kozi ya Wamama Wachungaji
Kozi ya uinjilisti ni kozi yetu inayotungwa kutimiza mahitaji ya wachungaji wasaidizi na wainjilisti.  Inatoa maelezo ya mambo ya misingi ya Biblia, Theolojia na Huduma. Wanafunzi wote wanapaswa kujifunza namna ya kuhubiri vizuri.
Kozi zetu za Diploma na Hati zinafuata silabus ya Jimbo la Kanisa la Anglikana Tanzania. Pamoja na hayo tunasisitiza masomo ya kuhubiri na Biblical Theolojia, yaani, Picha kubwa ya Biblia.  Wanafunzi wanapata mafundisho ya upana na kujifunza ujuzi mbalimbali wa kufanya huduma.
Tunao pia kozi ya kufundisha wake za wanafunzi wetu wa kozi za uchungaji. Kozi hii inawafundisha hawa wamama kuelewa na kufundisha Biblia pamoja na ujuzi mbalimbali kwa huduma za mama mchungaji. Kozi pia inafundisha ushonaji na ufundi mbalimbali.
 
Kozi zetu zote ni full-time na wanafunzi wanatakiwa kukaa chuoni. Kwa namna hii wanajifunza katika jamii ambayo ni namna bora kujifunza huduma.
Ada za Kozi hizi ni:
  • Diploma: 200,000/= kwa muhula.
  • Hati: 200,000/= kwa muhula.
  • Uinjilisti: 150,000/= kwa muhula.
Karibu sana!  Tumia ujumbe kwa maarifa zaidi.

Jipatie fomu ya kujiunga: Fomu  ya Usajili.

Mwanafunzi atakayepokelewa chuoni atakuja na ada pamoja na mapendekezo ya mchungaji wake au Askofu.
Pia naye kwa ushuhuda wa wanaomfahamu atafanana na tabia ya kiongozi wa kanisa kama inavyoandikwa katika 1 Tim 3, Tit 1 na 1 Pet 5.