Juu ya Chuo

Munguishi Bible College ni taasisi ya Dayosisi ya Mt Kilimanjaro kwa ajili ya kufundisha wachungaji na wainjilisti kwa huduma ya uchungaji.

Kwa utukufu wa Mungu tunafundisha wanafunzi kujua, kutegemea na kuihubiri Injili ya Yesu Kristo kuwa tumeokolewa kwa neema.

Munguishi ni chuo kinachosisitiza uanafunzi halisi wa Yesu — kumpenda Yesu na kutii neno lake, kumfahamu katika Neno la Mungu na kwa Roho Mtakatifu. Kozi zetu zinafundisha zote ufahamu na ujuzi wa huduma. Tuna mkazo wa kiinjili — kuweza kujua  Biblia na kuihubiri kwa uaminifu.

Kusudi la MBC

Munguishi Bible College inalenga kumtukuza Mungu kwa kufundisha watu kumhubiri Yesu Kristo kuwa Bwana kwa neno na tendo.  Tumejipa sharti kufundisha wanafunzi wetu kujua, kuamini na kufundisha Biblia; kuishi maisha matakatifu ambayo ni kielelezo kizuri; na kuwa viongozi wa kutumikia katika kanisa na jumuia.  Tunalenga kutayarisha viongozi watakaojitunza nafsi zao na mafundisho yao (1 Tim 4:16).

Maono

Kwa neema ya Mungu tunatumaini sana kuona wanaume, wanawake na watoto kuokolewa na jamii kubadalika kwa kutayarisha viongozi wenye utauwa kuhubiri Kristo bila hofu na kumfuata kwa uaminifu.